image carousel

Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Gabriella ni taasisi isiyo ya kiserikali ilioanzishwa Julai 2009 kuhakikisha watoto hawa wanatambuliwa mapema na kufundishwa kuwa wakukubalika kwenye jamii. Tunafanya Nini? Taasisi inashule ya msingi kwaajili ya watoto wenyeulemavu na wasio na ulemavu pamoja na shula ya bweni kwa wale wanaohitaji. Wataalamu wa therapi waliopo shuleni wakati wote pamoja na waalimu wanasaidia watoto wenye usonji na wenye matatizoo katika kujifunza. Wanatoa mafunzo kwa wazazi, walimu na jamii kwa ujumla kuongeza ufahamu juu ya ulemavu..

Sisi ni Nani

Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu kama ulemavu wa kimwili na matatizo ya akili ikiwemo Usonji cha Gabriella ni shirika lisilo la kiserikali (NGO)
iliyoanziashwa mwezi Julai mwaka 2009 kikiwa na malengo ya kuwatambua mapema,
na kuwapatia msaada wa mafunzo maalumu ya kitaalamu na kitabibu watoto wenye mahitaji maalumu kama walemavu wa kimwili na wale wenye matatizo ya akili kama Usonji, ili waweze kujitegemea na kukubalika katika jamii kama watoto wengine wasio na ulemavu.

Tunafanya Nini?

Kituo hiki maalumu kabisa kina shule maalumu yenye wataalamu waliobobea katika kutoa elimu na mafunzo kitaalamu kwa watoto wenye ulemavu wa kimwili na kiakili ikiwemo matatizo ya akili kama Usonji, na hata wale wasio na mahitaji maalumu! Pia kituo hiki kinatoa huduma maalumu ya malezi na malazi kwa watoto wanaohitaji huduma hiyo.

Katika kituo cha Gabriella, kuna watoa tiba kwa njia ya shughuli za kila siku (Occupational Therapists) wenye utaalamu wa hali juu kabisa ambao hushirikiana na walimu wenye ujuzi wa masuala ya watoto wenye mahitaji maalumu ambao kwa pamoja huwasaidia watoto wenye mahitaji maalumu wakiwemo wale wenye ulemavu wa viungo vya mwili, na Usonji kuweza kujifunza masuala mbalimbali ya kijamii na kielimu ili waweze kujitegemea katika masula mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Pia, wataalamu hao hutoa mafunzo kwa wazazi na walezi, walimu na wadau wengine katika jamii kuhakikisha kuwa wanaweza kuwahudumia watoto wenyeulemavu katika jamii zao kitaalamu.

Mission Statement

Kazi yetu ni kuendeleza na kutoa mazingira mazuri kwa vijana na watoto wenye ulemavu nchini Tanzania.Kuhakikisha kwamba wanathaminiwa na kutambuliwa ipasavyo ili kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maisha ya jamii.

Maono Yetu

Maono yetu ni kuishi Tanzania ambapo watoto na vijana wenye mahitaji maalumu wanaweza tumia uwezo wao wote katika maisha ya kila siku na kufurahia nafasi mbalimbali na kushiriki katika jamii moja kwa moja wakifanufaika pia na shughuli zao

PROGRAMU ZETU

WIKI MAALUM YA MAZOEZI

Huduma hii inalenga watoto wenye ulemavu wa akili ana viungo kuanzia umri wa 0 hadi miaka 0- 14 kwa kuwapatia fursa ya kumwona daktari bingwa wa watoto na kupata fursa ya mazoezi kutoka wataalum wetu. Ikitegemea hali ya mtoto mazoezi hutolewa kwa mfululizo au kwa kupishana inaweza kuwa kuanzia wiki moja hadi miezi 3. Pia mzazi au mlezi ana pata fursa ya kujumuika na wanzake an apia anapatiwa fursa ya kujifunzan anamna ya kuendelea na mazoezi nyumbani


Huduma ya awali ya kindagaten montesssori

Hii inaendeshwa siku za kazi kuanzia jumatatu mpaka ijumaa. Tunatoa huduma hii kwa watoto wenye uhitaji maaluma na wale wasiokuwa na uhitaji maalum. Mfumo wa Montessori hutumika kumsaidia mtoto kujifunza kwa kutumia milango yake Yote ya fahamu.ii inafanya kujifunza kuwe rahisi na kwenye kufurahiwa. Watoto wenye ulemavu wanapata fursa ya kuchangamana na wasikuwa na ulemavu .
Darasa la wenye mahitaji maalumu

Kituo cha Gabriella kina madarasa maalum kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye umri wa shule na hawajaweza kujumuika katika madarasa ya shule za kawaida. Wawapo kituoni wataalum wetu wanajaribu kutambua uwezo wao na namna yao ya kujifunza na hatimae kuweza kuwasaidia ile waweze kurudi shuleni jumuishi kwa wale wanaoweza. Madarasa haya pia yanakuwa mfano kwa namna ya kuwapatia watoto wenye uhitaji maalum elimu .

Uchunguzi na ushauri kwa watoto wa shule

Watoto walioko mashuleni wenye mahitaj mbali mbali kama vile kujifunza taratibu, wenye shida ya kusoma na kuandika. Tunawafanyia uchumguzi katika kituo chetu na pia wataalum wetu wanapokwenda kwa ziara za nje (outreach)
Darasa maalumu kwa watoto wenye usonji (autism).

Kituo cha gabriella kimebobea kuwasaidia watoto wenye usonji (autism). Kwa kuzingatia uhitaji wao gabriella ina darasa maalum ambalo lina wataalum wetu ambao wanaprogramu kwa kila mtoto . kwa njia hii watoto wenye usonji wanaweza kutambulika vipaji na uwezo wao.

Awareness Training

in the Aim of fighting stigma and realizing our vision.Gabriella centre has main focus on rising awareness about need and ability of peoplw with disability.

Gabriella has been leading fighting against stigma by working with other like minded organisation. we conduct workshop for parents, teachers, profesionals as well as community leaders. We organize and participate in 4 major events in rising awareness

1. International Kilimanjaro Marathon

2. World Autism awareness day

3. Africa Child

4. World day for People with disability

Outreach and home visits

Therapists and teachers conduct home visits to empower communities to realize their roles in supporting people with disabilities through conducting community awareness meetings and education sessions. The centre works with stakeholder such as churches,mosque,school and centres to allocate needed resources to people with disabilities. GABRIELLA has now extends the outreach to various areas in Kilimanjaro Arusha tannga and manyara regions, among many others!Kujifunza ujuzi

Huduma hii inalenga watoto na vijana wenye uhitaji maalum hasa wenye ulemavu na wale wanaotokea katika mazingira magumu. Inalenga kuwafundisha watoto ujuzi mbali wa kazi za mikono, shuguliiza za kila siku na stadi za maisha. Wataalum wetu wanatumia nja mbali mbali kufikia malengo haya. Watoto wachache wanapata pia fursa ya kukaa kituoni kujifunza kwa muda mfupi.

1. Shughuli wazojifunza ni pamoja na – ufugaji wa kuku, mbuzi, sungura

2. Bustani ya mboga, viazi lishe nk

3. Mapishi ya chakula, maandazi, karanga n.k

4. Ufundi cherehani – kutengeneza vitu vya culture kama mabegi, pochi n.k

5. Ufundi wa kuranda – vijana wanajifunza kutengeneza vitu mbali mbali hasa vinavyotuniwa na watoto wenye ulemavu

6. Kazi za mikono- hii inajumisha kutengeza vitu kwa shanga za kimasai kama vile bangili, herein , kobazi n.k

7. Uigizaji na ngoma – Sanaa ya uigizaji na ngoma inafundishwa kwa ajili ya kutambua na kuendeleza vipaji vya watoto na pia kujenga uwezo wa kujiamini

8. Utanashati- hii inalenga kutambua vipaji na pia kujenga uwezo wa kujiamini

Quality Test

Kituo kinatembelea jamii mbali mbali kwa nia ya kuwaweza kutambua jukumu lao katika kuwasaidia watu wenye ulemavu katika jamii. Pamoja na kuwatambelea pia tunaendesha mikutano mbalimbali

JINSI YA KUSAIDIA

UNAWEZAJE KUSAIDIA

Kituo kina shule ya msingi kwaajili ya watoto walemavu na wasio walemavu, pamoja na shule ya bweni kwa wanaohitaji.

Make a Donation
Volunteer with Us
Support a Child
Tackle a challenge/ climb with Purpose
help with a Fundraising

PICHA

** Picha Zetu

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Maelezo yake..

Jina la Mradi

Timu

Mfumo wa timu unakuwezesha kukua kama mtaalamu

Brenda Shuma

Executive Director

Nimwindael Mdee

Mkurugenzi Msaidizi

Emanuel

therapy assistant

AHABU

SPECIAL EDUCATION TEACHER

Habari na Matukio

Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu kama ulemavu wa kimwili na matatizo ya akili ikiwemo Usonji cha Gabriella ni shirika lisilo la kiserikali (NGO)
iliyoanziashwa mwezi Julai mwaka 2009

Kupambana na umaskini

Kupiga vita unyanyapaa na chuki kwa ,Makundi maalumu (Special groups),, ikiwa ni pamoja na watu wenye ulemavu Afrika na hasa watoto wenye usonji (autism), kituo cha kuwahudumia watoto wenye mahitaji maalumu cha Gabriela (GCRC) kimeanzisha mradi mathubuti,

Soma Zaidi

SIku ya Mtoto wa Africa

Kituo cha Gabriella kilishiriki katika kuandaa na kuhudhuria sherehe za siku ya mtoto wa Africa mjini moshi.watoto wetu walionyesha maigizo kuelezea haki zao.

Kuomba Huduma

Mtu yeyote anaweza kuomba huduma kwa niaba ya mtoto au kijana, kwa hiyo tumetengeneza hii fomu kukurahisishia.

Kama unaomba huduma kwa niaba ya mtoto au kijana na si mlezi wa kisheria tunataka kufahamu ni kama ingekuwa basi mlezi wa mtoto au kijana anataarifa

Kuomba Bonyeza kifungo KUOMBA HUDUMA

KUOMBA HUDUMA

CHANGIA

Kituo cha kuwahudumia watoto wenye Mahitaji Maalumu cha Gabriella ni sehemu ya funded Go Campaign. Reach For Change & Tigo, YES Kilimanjaro, CAPDA and individual donation.


Mahitaji yetu ya sasa/**wish list

1. Msaada wa vifaa vya shule kwa watoto waliokuja katika kituo chetu

2. Msaada wa usafiri kwa watoto au vijana ambao una karama ya dola za Kimarekani 120

3. Msaada wa sare za shule kwa watoto

4. I Pad kwa darasa la watoto wenye usonji (autism)

5. Mishahara kwa watoa tiba (therapist), waalimu wa wenye mahitaji maalumu na matron

Kwaajili ya uhitaji tunapanua huduma zetu ili kuwa na kituo bora zaidi kinachojitosheleza. Tumechagua kiwanja na tunashukuru YES Kilimanjaro na kampeni ya GO ambao wameonyesha kuguswa na changizo na tayari wanaunga mkono kwa kununua hekari 5 za ardhi.

.

Waweza kushiriki kwa kumsaidia mtoto mmoja kupata nafasi ya kupata tiba(therapy) katika kituo cha Gabriella, kwa kulipia uwepo wao, vifaa vy tiba nk

Kwa maelezo zaidi na kujihusisha, wasiliana na

Brenda Shuma

brenda@gabriellarehab.org

gabriellacentre@hotmail.com

MSAADA WAKO UKO SALAMA KUPITIA HUDUMA YA PAYPAL..

Wasiliana Nasi

Kwa habari zaidi na kujihusisha,wasiliana nasi.

Mawasiliano

Gabriella Children’s Rehabilitation Centre
P.O. Box 9626, Sambarai Kibosho Road
Tanzania
Simu: +255 (0) 713202654 Email: gabriellacentre@hotmail.com@gmail.com Website: www.gabriellarehab.org